C & P

SABABU INAYOFANYA WABABA KUFA MAPEMA!!🇹🇿

Baba anapokuwa bado ana nguvu, yuko kazini huwa anakua na nguvu na ushawishi mkubwa sana kwenye familia yake, familia humsikiliza, huzingatia uwepo wake!
Tatizo huanza pale baba anapozeeka, nguvu za uzalishaji mali zimekwisha, amestaafu! Na pale watoto wanapokua wamekua watu wazima wameanza maisha yao! Hapo ndipo mambo kwa baba humgeuka!
Mkewe huanza kumchukulia poa! Ile heshima aliyokuwa akipewa huanza kupungua taratiib.. baba hasikilizwi tena Kama zamani, isitoshe anakua hahusishwi sana tena kwenye mambo ya mkewe sababu hata akiambiwa atasaidia nini na pesa hana?
Badala yake mkewe huanza kuwafanya watoto kuwa washirika wake zaidi na kumuweka kando mumewe... Baba anaachwa pembeni!

Mama huanza safari kwenda kwa watoto, huko hukaa sana, baba kaachwa nyumbani peke yake! Watoto wanagombea mama aende kwao, lkn baba hakuna anayemtaka!
Wakiwa nyumbani na mkewe, simu toka kwa watoto 80% anapigiwa mama, baada ya maongez mareefu, ndo baba anapewa simu anasalimiwa dk 2 imeisha hiyo! Baba simu anayo, ila haoni simu za watoto wakimpigia, na wakimpigia ni kwa sababu maalumu tena maongez huwa mafupi! Hawana muda nae!
Baba anajikuta anakuwa mpweke sana, anakua mgeni kwa familia yake mwenyewe! Wale ambao alizimalizia nguvu zake za ujana kuwatafutia hawana muda nae!
Pale baba anapokuwa anaihitaji sana faraja ya familia yake sababu ameshazeeka... Familia humpa kisogo! Upweke unamsonga! Sababu ya upweke mawazo humsonga, hili hupelekea kinga ya mwili kushuka na kufanya iwe rahisi kushambuliwa na magonjwa na haichukui muda anafariki!
Familia wataliaa, watachapisha matisheti, watatoa mapesa kumnunulia sanduku la gharama na kumjengea kaburi la gharama, mitandaoni watampost sana! Lakini alipokuwa hai... No one cares!
Tuwajali baba zetu, walijitoa na kujinyima sana kufanya tufike tuliko! Ni dhambi mbele za Mungu tena ni laana mbaya kuwapuuza baba zetu!
You can follow @Malakasiq_Jr.
Tip: mention @twtextapp on a Twitter thread with the keyword “unroll” to get a link to it.

Latest Threads Unrolled:

By continuing to use the site, you are consenting to the use of cookies as explained in our Cookie Policy to improve your experience.