👉UONGOZI: ni mamlaka au karama ya kuwaonyesha watu njia kwa vitendo.
👉Kipimo cha uongozi ni jinsi gani kiongozi anaweza kuleta ushawishi kwa watu na kufikia maendeleo yaliyotarajiwa.
👉Kiongozi bora hana muda wa kulalamika bali anatafuta ufumbuzi wa matatizo ya wananchi au watu
walio chini yake.
👉Kiongozi wa kweli akiongea, watu husikiliza.
#77nyeupe #TumeHuruYaUchaguzi
#msajiliwavyamavyasiasa #thankmelater
👉Kuna njia nyingi za kuainisha uongozi lakini njia ya msingi ni kuangalia jinsi kiongozi alivyoingia madarakani na utaratibu wake wa kuongoza.
👉Katika viongozi wapo Wafalme, Marais, Mawaziri, Watemi, Machifu, Wakurugenzi n.k.
👉Viongozi hawa wote tunaweza kuwagawa katika
mafungu yafuatayo kutokana na jinsi walivyoingia madarakani na namna wanavyoongoza kama ifuatavyo:
👉Wale wanaopata uongozi kwa kurithi.
👉Wanaopata uongozi kwa kuchaguliwa.
👉Wanaojitwalia mamlaka ya kuongoza kwa nguvu.
👉 Wanaoteuliwa na mamlaka za juu zaidi.
👉Kiongozi anayeingia madarakani kwa mojawapo ya njia zilizotajwa hapa juu anaweza kutumia mtindo wake wa uongozi.
Ipo mitindo mbalimbali ya uongozi:
👉Uongozi wa kimila
👉Uongozi wa kidemokrasia.
👉Uongozi wa kiimla ni mtindo wa kuongoza ambao kiongozi huongoza kwa amri bila kushirikisha watu wengine katika kufanya maamuzi. Mara nyingi uongozi wa aina hii haulengi katika kukidhi maslahi ya
ya walio wengi, bali tu ya yule anayeongoza na wale wanaomlinda.
👉Uongozi wa kidemokrasia ni ule wa kushirikisha watu katika kufanya maamuzi na utekelezaji wake. Kwa kawaida viongozi wa aina hii hulenga kukidhi mahitaji ya walengwa.
👉Viongozi wanaochaguliwa mara nyingi huwa..
huwa wanapewa muda wa kuongoza, na wale viongozi wanaojiteua hujipatia wao wenyewe muda wa kuongoza au hata hapo watakapoamua kuachia madaraka.
You can follow @annashocky.
Tip: mention @twtextapp on a Twitter thread with the keyword “unroll” to get a link to it.

Latest Threads Unrolled:

By continuing to use the site, you are consenting to the use of cookies as explained in our Cookie Policy to improve your experience.