story time:
Kuna daktari mmoja alikuwa anasoma SUA(Vet), jina lake ni Frank. Kwa mujibu wa wanawake waliomuona live au kwenye picha wanasema ni bonge la handsome. mimi kwangu alikuwa ni mshikaji sana, mcheshi na mtoa support kwa wana.
Frank alikulia mazingira ya kishua flani.
Kuna daktari mmoja alikuwa anasoma SUA(Vet), jina lake ni Frank. Kwa mujibu wa wanawake waliomuona live au kwenye picha wanasema ni bonge la handsome. mimi kwangu alikuwa ni mshikaji sana, mcheshi na mtoa support kwa wana.
Frank alikulia mazingira ya kishua flani.
Primary, O’level na Advance jamaa alikuwa. akishobokewa sana na warembo hadi kufikia hatua wana wanamchukia. Frank hakujali maana hawezi kucontrol hiyo hali, na pia yeye anafuatwa si anakuwa mkarimu tu(warembo waliliwa wengi tu). Sasa alipofika chuo ndo mambo yakawa HOT
.

Mwaka wa kwanza sem1, jamaa anakanyaga chuo tu hata wiki bado warembo wanashoboka. akanipigia mwanae like “oya mwanangu, SUA kuzuri kinoma”, mi nikahisi anamaanisha mazingira. Nika-support mada na story zikaendelea kiaina then akaaga. class lake lina-wadada 10 tu, afu kawaida tu.
sasa kuna mrembo mmoja wa kuitwa Nurat alikuwa mwaka wa kwanza pia kozi tofauti na ya Frank. Jamaa alimuona mara ya kwanza pale utawala sijui alifuata nini mshikaji maana sio pigo zake(ye akishalipa ada, hataki kung’aa pande hizo). Frank akapishana na toto la hatari mzeeee

Akasimama kwanza na kuvunja shingo, akaduwaa, akapiga picha afu akasepa zake. Akarudi room kwake akamuuliza mshikaji, “oya unamsoma huyu mtoto”, jamaa akamwambia hapana. Frank akaumia moyo ila akasema ipo siku atamkuta tena.
Punde si Punde akakutana nae tena, this time ni cafe.
Punde si Punde akakutana nae tena, this time ni cafe.
Jamaa akapiga nae story 2/3 pale, akachukua digits then akasepa room. Frank alifurahi na hakutegemea kama zoezi gumu lingekuwa jepesi vile. Kosa alilofanya Frank ni kumtafuta yule demu siku ileile na ilikuwa night.
Fra: mambo?
Nur: poa.
Fra: naitwa Fra
Nur: aha, mbona saa hizi?
Fra: mambo?
Nur: poa.
Fra: naitwa Fra
Nur: aha, mbona saa hizi?
Fra: nimeona nikusalimie.
Nur: kwani ungengoja hadi kesho ungekufa?
Jamaa moyo ukapasuka na kufokewa kule, akaaga akalala zake
.
maisha yakaendelea huku akiendelea kupiga sound kwa mtoto na kugalagazwa vizuri tu. yule mtoto alitolewa macho na kila mwanaume pale SUA.
Nur: kwani ungengoja hadi kesho ungekufa?
Jamaa moyo ukapasuka na kufokewa kule, akaaga akalala zake

maisha yakaendelea huku akiendelea kupiga sound kwa mtoto na kugalagazwa vizuri tu. yule mtoto alitolewa macho na kila mwanaume pale SUA.
Sasa unaweza pata picha kwamba Frank anashobokewa na wanawake kibao ila hawataki kwa muda huo, anamtaka Nurat. Nurat anashobokewa na wanaume kibao, ila hawataki wote. Frank akafuatilia info za Nurat, akaja kujua kuwa na yeye ni wa kishua sana, tena zaidi yake. Frank hakufa moyo.
Frank akasema hapa kuhonga hakufai, outing za kawaida nitaumbuka. Siku ya siku Frank alijipanga kumuomba Nurat watoke kwenda sehemu flani, which aliamini atakataliwa tu. Akiwa njiani kwenda kwa Nurat, kuna Prado nyeusi ikampita kama upepo na kumuachia vumbi ikielekea anapoenda.
Frank akatukana kimoyomoyo(fala nini, utafilisika tu), akafika zake Hostel akapanda gorofani. Wakakutana uso kwa uso na Nurat akitoka, akamsalimia Frank na kumwambia mi natoka na mume wangu mtarajiwa, labda uje kesho maana sirudi leo. Frank moyo paaaaaaa, na akaishiwa nguvu
.

Akamcheck mtoto akishuka, akafika kwenye ile Prado jamaa akashuka(kipande), akampa wet kiss refu tu. mtoto akaingia kwenye ndinga wakasepa wakiacha vumbi machoni mwa Frank. Hakuwahi kupenda mwanamke kama hivi, aliangusha chozi. Frank akajisemea “Karma is doing her dirty work”.
Wakati Frank akipiga harakati zake za kumnyakua Nurat, kumbe kuna jambo lingine likiendelea upande wa pili bila yeye kujua. kunae hilo toto lingine lilikuwa linaitwa Rebecca. Mfupi flani, kajaa matata, mguu ni tembo na hapo nyuma kunastahili thread yake kabisa. Frank na ngekewa.
Rebecca alikuwa haelewi kwa Frank, yaan alishatuma marafiki ila jamaa akawa anapuuzia. Siku wakamuita mahali, bila kujua akaenda. Wakamkutanisha na Rebecca na kumwambia mnatakiwa kuongea, Rebecca alifunguka ya moyoni pale weee jamaa anasikiliza. Frank akaona ni mzuri, smart, etc.
ila ndo vile hajamuelewa. Rebecca akaaga, akiwa anaondoka Frank akaona baraka za Rebecca. Mwanangu Frank akabaki njia panda sasa, maana ugonjwa wake ni huo na ukichanganya na akili za Rebecca basi akawa na mawazo sana. Frank akanipigia simu, akanielezea yote na jinsi anavyowaza.
nikampa jibu moja tu “follow your heart bro”. Rebecca akawa anakaba hadi penati kwa Frank, maana alikuwa anajua connection ya Frank na Nurat so alikuwa anakomaa kuvunja ile hali. Rebecca akaomba waende dinner(kwao hamna njaa pia), jamaa akakubali. wakaenda dinner, wote walienjoy.
1st yr ikaisha, 2nd yr wakarudi kuendeleza gurudumu. Frank akawa anajilazimisha kuwa na Rebecca ingawa akimuoma Nurat huwa anaishiwa nguvu kabisa. 2nd yr ikikaribia kuisha, Frank akaanza kuzoea kuwa Nurat hamtaki na anatakiwa anendelee na maisha na aache kumtesa Rebecca.
likizo ya 2nd yr wakaondoka wote chuo, coz wanaishi Dar wote. Wakapanda zao Abood bus, wakaenda zao mjini likizo. ofcoz walipokuwa likizo walikuwa pamoja muda mwingi, ilifanya bond yao kuwa strong zaidi. Frank akaanza kumpenda Rebecca ile serious taratiiiibu. likizo ikaisha.
3rd yr(sio 3th bana), wakarudi chuo wakiwa wapenzi kamili. Sasa kulala hostel kukawa mara chache sana, wao ni lodge na hotels tu wanakula kuku(si wote wakishua, pesa ipo). sem2 Rebecca akapata ujauzito, bahati nzuri hadi anamaliza 3rd yr haikumsumbua na akafanya UE fresh kabisa.
Rebecca akagraduate huku Frank akiendelea na shule. Rebecca akapata kazi Dar, ila kila weekend yuko Moro anamletea utamu wake Frank. Frank hakutegemea kama Rebecca ni smart, loving, caring, supportive woman kiasi kile. Kwa asilimia kubwa Rebecca alikuwa anamsupport Frank.
Frank akamaliza chuo pia, kipindi akiwa hana kazi Rebecca alikuwa anafanya kila kitu pale home na akamkataza kuomba pesa kwa wazazi coz yeye anafanya kazi. Frank akamchumbia Rebecca, baada ya miezi kadhaa akamuoa wakiwa na mtoto mmoja fresh tu. Frank akawa mtu mpya kabisa

Sasa hivi anawatoto 2, anakituo chake cha mifugo na maisha ni mazuri. Rebecca anaenjoy maisha na mwanaume anayempenda mno.
Nurat nae ameolewa na yule jamaa wake wa Prado, maisha yao ya raha yanaendelea kama kawaida.
Frank ameshamsahau Nurat na sasa anakula maisha matamu.
Nurat nae ameolewa na yule jamaa wake wa Prado, maisha yao ya raha yanaendelea kama kawaida.
Frank ameshamsahau Nurat na sasa anakula maisha matamu.
FUNDISHO:
Kukataliwa na umpendae sana sio mwisho wa kuenjoy mapenzi. Kuwa mvumilivu huku ukitafuta njia zako, utaletewa wa kufanana nae wa maisha.
Usimuombee mabaya aliyekukataa bali muombee baraka na wewe utabarikiwa.
Kukataliwa na umpendae sana sio mwisho wa kuenjoy mapenzi. Kuwa mvumilivu huku ukitafuta njia zako, utaletewa wa kufanana nae wa maisha.
Usimuombee mabaya aliyekukataa bali muombee baraka na wewe utabarikiwa.